Compare Properties

Compare
You can only compare 4 properties, any new property added will replace the first one from the comparison.House Purchase

Purchasing process

HATUA ZA KUMILIKI KIWANJA:

1. Fika ofisi za halimashauri ya jiji la Dodoma Au ofisi za Hans Mult Consult Co Ltd kujaza fomu ya maombi ya kiwanja.

2. Baada ya kujaza fomu ya maombi utachagua kiwanja kutoka kwenye ramani zilobandikwa kwenye mahema yaliyopo viwanja vya wazi katika ofisi za zamani za manispaa ya Dodoma.

3. Baada ya kujaza fomu utapewa bili ya malipo (invoice) kwa ajili ya kuanza kulipia kiwanja chako kwa muda wa miezi 3.

4. Baada ya kumaliza malipo yote ya kiwanja kama ilivyoelekezwa kwenye bili ya malipo utafunguliwa faili lako kwa ajili ya maombi ya kuandaliwa hati ya kumiliki kiwanja.

5. Hati yako ya kumiliki kiwanja itakamilika ndani ya siku 21 tangu kufunguliwa kwa faili lako la maombi ya hati.HATUA ZA KUMILIKI NYUMBA YAKO:

1. Muombaji anatakiwa awe anamiliki kiwanja chake halali,kama hana kiwanja Hans Mult Consult Company Limited Watamsaidia kutafuta kiwanja kulingana na na uwezo wake na mahali anapopenda kisha atalipia baada ya makubaliano na mwenye kiwanja.

2. Muombaji atajaza fomu katika ofisi za Hans Mult Consult Co Ltd (Dodoma) au anaweza download kwenye website yetu (www.hansmc.co.tz).

3. Muombaji atarudisha fomu ya maombi ofisi za Hans Mult Consult Co Ltd au atatuma kwenye anuani yetu (S.L.P 4198, Dodoma) akiambatanisha na nakala za nyaraka za umiliki.

4. Tutapitia maombi ya muombaji kwa pamoja na kutembelea eneo la ujenzi kuthibitisha eneo lilipo, ukubwa wa eneo, umiliki halali na mazingira ya kiwanja kilipo.

5. Baada ya kujiridhisha muomba atalipia 50% ya jumla za gharama za nyumba aliyochagua kisha kusaini mkataba kati yake na Hans Mult Consult Company Limited.

6. Nyumba itajengwa na kukamilishwa ndani ya miezi mitatu (3) kisha muombaji atakabidhiwa funguo ikiwa nyumba imekamilika kama ilivyoelezwa kwenye mkataba na muombaji kumalizia 50% iliyobaki.